SIMBA NA YANGA KUGOMBEA MILIONI 100 ZANZIBAR

KAMATI ya Kombe la Mapinduzi, imetangaza rasmi kwamba, bingwa wa michuano hiyo ataondoka na kitita cha shilingi milioni 100, huku mshindi wa pili kukabidhiwa shilingi milioni 70 na vilabu vya Simba na Yanga vitakua moya ya timu zitakazowania kitita hicho.

Mashindano hayo ambayo yanatarajiwa kuanza Desemba 28, mwaka huu, yatashirikisha timu 12, huku msimu uliopita bingwa ambaye alikuwa Mlandege, aliondoka na shilingi milioni 50.simbaMwenyeketi wa Kamati ya Mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Mbarouk Othman, amesema siku ya ufunguzi, itachezwa michezo miwili kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Amesema timu za Bandari ya Kenya na URA ya Uganda, zimejitoa katika mashindano hayo na nafasi zao zimechukuliwa na Jamuso kutoka Sudan Kusini na JKU ya Zanzibar.

Acha ujumbe