Kikosi cha Simba Queens kinatarajia kuondoka kesho Jumanne kuelekea Morocco kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa Afrika wakiwa wanaiwakilisha Kanda ya Afrika Mashariki na Kati.

Hayo yalisemwa na meneja wa Simba Queens Seleman Errasy Makanya ambaye alisema wanatarajia kuondoka usiku wa Oktoba 25 na kufika Morocco Oktoba 26 na wanaweza kupitia Uturuki au Dubai ambako wataunganisha ndege.

Simba, Simba Queens Safari ya Morocco Imeiva, Meridianbet

Makanya alisema: “Tunatarajia kuondoka Oktoba 25 usiku na tutaingia kule Oktoba 26, nafikiri tunaweza kupitia Dubai au Uturuki. Tunahitaji kufika kule na kupata muda kidogo wa kujiandaa na kuzoea mazingira.”

Simba wamepangwa kundi D na klabu za AS FAR ya Morocco, Green Buffalo ya Zambia na Determine Girls ya Liberia na mashindano hayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Oktoba 30 hadi Septemba 15.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa