Simba Queens Kibaruani Kesho

Klabu ya Simba Queens watashuka tena uwanjani kesho Jumamosi nchini Morocco kucheza mchezo wa kusaka mshindi wa tatu dhidi ya Bayelsa Queens kutoka Nigeria.
Kocha wa timu hiyo Charles Aex Lukula amesema kuwa wao hawana presha yoyote ya kuelekea kwenye mchezo huo kwa sababu wanafahamu wana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutoka na maandalizi yao.

“Hatuna presha hata kidogo kwa sababu tunajiona tupo kwenye nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo. Vijana wapo saw ana wanaona inawezekana kutorudi nyumbani patupu,” alisema Lukula.
Simba walitinga nusu fainali kwa mara ya kwanza kwenye historia yao baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya mabingwa watetezi Mamelody Sundowns Women FC kwa bao 1-0.
Watavaa na Bayelsa Queens ambao walifungwa bao 1-0 na AS Far Rabat kwenye mchezo wa nusu fainali. Mechi ya mshindi wa tatu na fainali zote zinatarajiwa kuchezwa leo Jumamosi.

Acha ujumbe