Mabingwa wa CECAFA na wawakilishi wa Ukanda huo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa wanawake barani Afrika, Simba Queens watakutana na timu ya wanawake ya Mamelod Sundowns Queens ya Afrika Kusini ambayo ni mabingwa watetezi wa mashindano hayo.

 

Simba Queens Kucheza na Mamelod Sundowns Nusu Fainali

Simba Queens wamefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali baada ya kuwaondosha Green Buffaloes ya Zambia kwa magoli 2-0, na hivyo kuandika rekodi mpya ambayo haijawahi kuwekwa na timu yeyote kutoka Tanzania.

Awali Ilitegemewa Simba Queens atakutana na Timu ya wanawake wa TP Mazembe lakini sasa, watakutana na miamba hiyo ya Afrika kusini ambao ni mabingwa watetezi, na TP Mazembe atakutana na kinara wa kundi A, AS FAR ya nchini Morocco.

 

Simba Queens Kucheza na Mamelod Sundowns Nusu Fainali

Mchezo wa nusu fainali katika ya Simba Queens na Mamelod utachezwa siku ya Tarehe 09/11/2022.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa