Kesho kutwa Jumatano Simba Queens watashuka dimbani kucheza mechi ya nusu fainali na mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita Mamelody Sundowns.

Simba watashuka dimbani kucheza mchezo huo ikiwa ni mara ya kwanza wanafika kwenye hatua hiyo. Simba walikusanya alama sita kwenye kundi A nyuma ya AS Far.

Simba Queens, Simba Queens Kusaka Rekodi Nyingine Kesho Kutwa, Meridianbet

Mchezo mwingine wa nusu fainali hiyo kesho ni kati ya majirani wa Tanzania TP Mazembe kutoka DR Congo, ambao watacheza na AS Far.

Kocha wa Simba, Charles Alex Lukula alisema kuwa: “Hatuna cha kupoteza kwenye mchezo huo, ingawaje kila mmoja wetu anajua kuwa tunakwenda kukutana na timu bora na bingwa wa mashindano haya.

“Tutajitolea kwa kila namna sisi kama makocha kuhakikisha tunawakumbusha vijana kuwa umuhimu wa kushinda mechi hii ni mkubwa sana.”

Opah Clemant, nahodha wa timu hiyo alisema kuwa: “Sisi tupo tayari kwa mchezo huo ambao unakwenda kuwa mgumu. Tupo tayari kwa kila kitu na ninaimani tunakwenda kushinda.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa