Simba Queens Yaifuata Green Buffaloes

Kikosi cha Simba Queens kimesafiri asubuhi ya leo kuelekea mjini Marrakech kwaajili ya mchezo wao wa mwisho hatua ya makundi dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia.

Mchezo huo utapigwa kesho Novemba 5, 2022 na ndiyo utahitimisha ratiba ya makundi na kuweka hatma ya Simba Queens, ambao ni wawakilishi pekee kwa ukanda wa CECAFA.

 

Simba Queens Yaifuata Green Buffaloes

Mchezo wa kwanza wa Simba alipoteza dhidi ya wenyeji AS FAR kwa bao 1-0, na kuwafanya kupoteza alama tatu muhimu ambazo zingewafanya wawe kwenye eneo zuri, lakini kwenye mchezo wa pili walijipapatua na kupata ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Determine Girl kutokana nchini Liberia.

Kocha Mkuu wa Simba Queens Charles Lukulu alisema kuwa ‘nguvu zote wanazielekeza kwenye mchezo wa kesho’

 

Simba Queens Yaifuata Green Buffaloes

Ili Simba wafuzu hatua inayofuata, itawalazimu kushinda mechi yao ya kesho dhidi ya Green Buffaloes kwani wote wana alama 3 hivyo mshindi wa kesho ataungana na mwenyeji, AS FAR kwenye hatua inayofuata, ambapo hajapoteza mechi hata moja mpaka sasa.

Acha ujumbe