TIMU ya Wanawake Simba Queens imewasili salama mjini Rabat kuvaana na Mamelod Sundowns Queens wakitokea mji wa Marrekech, walipokuwa kwenye mechi yao ya mwisho iliyopatia tiketi ya kucheza nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa upande wa wanawake ambayo yanafanyika nchini Morocco.

 

Simba Queens Yarejea Rabat Kucheza na Mamelod

Mchezo huo wa kwanza wa Nusu fainali utapigwa majira ya saa 11:00 kwa saa za Morocco, kwa hapa Tanzania na Afrika Mashariki itakuwa ni saa 1:00 usiku. Kwa mara ya kwanza kwenye historia ya soka la wanawake Simba Queens anaenda kuandika rekodi usiku wa Jumatano Novemba 09, 2022.

Nahodha wa Mabingwa hao wa Ligi ya Wanawake Tanzania, na Mabingwa wa CECAFA msimu huu wa 2022, Opah Clement alisema kuwa wachezaji kwa upande wao wamejiandaa vizuri na wana kiu ya kucheza fainali za Ligi ya Mabingwa.

 

Simba Queens Yarejea Rabat Kucheza na Mamelod

Simba Queens wamefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali baada ya kuwaondosha Green Buffaloes ya Zambia kwa magoli 2-0, na hivyo kuandika rekodi mpya ambayo haijawahi kuwekwa na timu yeyote kutoka Tanzania.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa