DIRISHA la usajili lipo wazi na kila timu yenye nguvu sokoni imekuwa ikipambana kusaka wachezaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao, kati ya timu ambazo zimeanza kwa kasi kwenye ishu ya kusajili ni Simba. Simba imeshatambulisha wachezaji wapya kama Nathaniel Chilambo akitokea Azam FC, Bakari msimu aliyetokea Coastal Union, Kelvin Nashon kutokea Pamba na huku wakimuongezea mkataba mpya, Seleman Mwalimu.
Wakati huo huo Simba inatajwa ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha usajili wa mshambuliaji hatari raia wa Mali, Ibrahim Doumbia, ikiwa ni katika harakati za kuboresha na kujenga kikosi imara zaidi kwa ajili ya msimu mpya wa ligi. Inaelezwa kuwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 tayari amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya afya kabla ya kuweka saini kwenye mkataba rasmi wa kujiunga na Wekundu wa Msimbazi.
ligi kuu tanzania, nbc premier league, ligi kuu bara, odds za kubeti ligi kuu NBC, mechi za ligi kuu Tanzania, ligi kuu ya NBC,
Doumbia anajiunga na Simba akitokea klabu ya AS Kôrôfina inayoshiriki Ligi Kuu ya Mali, ambako alikuwa na msimu wa kipekee uliomweka miongoni mwa washambuliaji hatari zaidi nchini humo. Doumbia kwenye msimu uliopita alihusika kwenye mabao 22 katika mechi 24 alizocheza na aliibuka kuwa mfungaji bora, akifunga mabao 17 na kutoa pasi 5 za mabao.
Mbali na kutwaa kiatu cha ufungaji bora wa ligi, Doumbia pia alitwaa tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi wa Msimu nchini Mali, jambo lililowavutia vigogo wengi barani Afrika kabla ya Simba kufanikiwa kushinda vita ya saini yake. Akizungumzia mipango ya usajili Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Ahmed Ally alisema: “Lengo letu ni kuhakikisha tunakuwa na timu bora zaidi msimu ujao, tunasajili wachezaji wenye sifa ya kucheza Simba na kuipa mafanikio timu yetu, dhamira yetu ni kushinda vikombe na kurejeha heshima yetu.”
Kukamilika kwa usajili wa mshambuliaji huyo kutaongeza ushindani mkubwa na chachu ya mabao katika safu ya ushambuliaji ya Simba, inayojiandaa na vita ya kusaka mataji ya ndani ikiwemo Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Shirikisho, pamoja na mashindano ya kimataifa. Mashabiki wa Simba sasa wanasubiri kwa hamu tangazo rasmi kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo pindi taratibu za vipimo vya afya na usajili zitakapokamilika na mchezaji huyo kutangazwa rasmi kuwa mali ya timu yao.


