Kocha wa Simba SC Juma Mgunda Maarufu kama Pep Guardiola wa Bongo, mara baada ya kupata ushindi wa magoli 2-0 wakiwa ugenini, dhidi ya Nyasa Big Bullets kwenye mechi ya kwanza ya mashindano ya klabu bingwa amesema kuwa bado mechi haijaisha.

 

Simba SC Bado Mechi Haijaisha Mgunda Anena.

Akizungumzia mchezo huo, kocha Mgunda alisema kuwa mchezo haujaisha kabla ya kuisha, kuna mechi ya pili itachezwa Dar Es Salaam, najua kuna makosa yalijitokeza kwenye mechi hii, lakini tutayarekebisha kabla ya kucheza mechi ya pili na naamini tutashinda.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Fatmalikwata (@fatmalikwata)


“Niliongea na wachezaji ili watambue haki na wajibu wao, na wao walikuwa wanajua mashabiki na wapenzi wanataka nini, hivyo wachezaji ndio watekelezaji wa mwisho”

“Mwalimu niliyemkuta nilishawahi kufanya nae kazi kwenye timu ya taifa kwa miaka miwili au mitatu, naujua uwezo wake na timu ilikuwa kwenye mikono salama. Nichukue nafasi hii kumshukuru Mwalimu Matola amenisaidia sana mpaka kuhakikisha leo tunafanya vizuri”Mgunda Alifafanua.

Simba SC Bado Mechi Haijaisha Mgunda Anena.

Wanalunyasi, wanapata matokeo dhidi ya mabingwa hao kutoka nchini Malawi mara baada ya kulazimishwa suluhu katika mchezo wao wa ligi kuu Tanzania bara, na klabu ya KMC Jijini Dar-es-salaam.

Simba SC ambao wamekua wazoefu katika michuano hiyo, walipata goli lao la uongozi kupitia kwa mshambuliaji wao raia wa Zambia Moses Phiri, akiwa anafunga goli lake la nne, katika michezo minne aliyocheza hadi sasa huku goli la pili likifungwa na nahodha wa timu hiyo mkongwe John Raphael Bocco.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Azam Sports (@azamtvsports)

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Azam Sports (@azamtvsports)

Simba SC inapata matokeo mazuri ikiwa ugenini kitu ambacho kinaweza kuwakikishia kusonga mbele kwenye hatua kwanza ya michuano hiyo. kwani imekua nadra sana kwa klabu hiyo kupoteza mchezo wakiwa katika dimba lao la nyumbani.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa