KLABU ya Simba SC katika kujiimarisha kwenye safu yao ya Ushambuliaji, Taarifa za chini ya buswati zinasema kwamba wanafuatilia mwenendo wa straika anayekipiga kwenye timu ya Najran ya nchini Saudi Arabia ili kumsajili kwenye dirisha dogo.

 

Simba SC Kusajili Mshambuliaji Mghana

Mchezaji huyo ambaye ni raia wa Ghana anafahamika kwa jina la Kwame Opoku mwenye umri wa miaka 23, kwa sasa anaichezea Ligi ya Saudia ambapo Simba wanamfuatilia kwa karibu zaidi chini ya wakala wake, Alpha Sports Management Ltd, ili kuongeza ufanisi eneo la ushambuliaji la timu.

Eneo la ushambuliaji kwa sasa linaongozwa na Moses Phiri, Clatous Chama, Pape Sakho, Agustine Okrah, Habib Kyombo, John Bocco na Kibu Denis Prosper.

 

Simba SC Kusajili Mshambuliaji Mghana

straika huyo amewahi pia kuichezea Asante Kotoka ya kwao Ghana, kwa sasa yupo Najran kwa mkopo kutoka kwa wababe wa soka wa Algeria USM Alger, na kabla ya kujiunga na Asante Kotoko pia amewahi kuichezea klabu ya NKZ Warriors SC.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa