Simba SC Yatambulisha Mbrazil-Roberto Oliveira

Klabu ya Simba SC mapema hii imemtambulisha kocha mpya Roberto Oliveira (Robertinho) kuwa kocha mkuu, nafasi iliyokuwa inashikiliwa kwa muda na Juma Mgunda.

 

Roberto Oliveira

Kocha huyo mpya ni raia wa nchi yenye vipaji vingi vya soka na mabingwa mara 7 wa kombe la dunia, Brazil ambapo kabla ya kujiunga na Simba SC alikuwa akiifundisha klabu ya Vipers ya Uganda ambao alivunja nao mkataba hivi karibuni.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa Roberto Oliveira alisema kuwa amepewa malengo makubwa ya kuisaidia Simba SC kufika mbali kwenye klabu bingwa CAFCL.

 

simba

“Nimekubaliana na changamoto mpya. Ukiwaza makubwa unafanya makubwa, malengo ni kufika Nusu Fainali na hata fainali, inawezekana.”- Roberto Oliveira

Kwa maana hiyo ni rasmi sasa, kocha Mgunda ataenda kuwa msaidizi wa Roberto Oliveira huku Mkongwe Seleman Matola yeye akisalia klabuni hapo lakini kwa sasa ana jukumu la kujiendeleza kielimu zaidi.

Acha ujumbe