Kikosi cha Simba kiliwasili siku ya jana nchini Sudan kwa mualiko maalum kutoka kwa wenyeji wao Al Hilal ambao wamewaalika Simba kucheza mechi mbili za kirafiki.

simba, Simba SC Waacha Kufanya Maozezi Kupisha Adhana., Meridianbet

Wakiwa Sudan, Simba waliendelea na ratiba yao ya kufanya mazoezi ambapo jumla ya wachezaji 19 walisafiri huku nyota wengine 8 wakiwa wameitwa kuitumikia Taifa Stars ambayo watamenyana na Uganda kufuzu CHAN tarehe 28 Agosti.

Matukio Yaliyojitokeza Siku ya Kwanza ya Mazoezi ya Simba.

Onyango hajaonekana mazoezini.

Wakati timu inafanya mazoezi kati ya wachezaji walionaswa na kamera ni wachezaji Chama, Inonga, Okrah, Okwa, Sakho, Banda, Akpan, Gadiel, Mwanuke, Ally Salim, Kapama, Dejan, Outtara, Phiri na wengine lakini cha kushangaza ni kwamba Joash Onyango hayupo Sudan na imebainika kabaki Dar Esalaam huku kwa taarifa ambazo sio za kuaminika inasemekana anataka kuvunja mkataba wake na Simba.

simba, Simba SC Waacha Kufanya Maozezi Kupisha Adhana., Meridianbet

Mazoezi Yasimama kwa Muda Kupisha Adhana.

Wakiendelea na mazoezi ilitokea hali ambayo wachezaji wa Simba pamoja na viongozi wengine walisimamisha mazoezi yao kupisha Adhana kuadhiniwa na kuwapa fursa wachezaji wa Iman ya Kiislam kuswali.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania)

Simba watacheza michezo hiyo miwili ya kirafiki na Asante Kotoko ya Ghana na pamoja na wenyeji wao Al Hilal, huku mchezo wa kwanza akitarajia kucheza Agosti 28 dhidi ya Asante Kotoko na 31 Agosti dhidi ya Al Hilal.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa