Simba SC Yawafuata Asante Kotoko na Al Hilal ya Sudan.

Ilikuwa ni majira ya saa 10 ya Alfajiri ya leo ambapo wachezaji 19 na viongozi wa Simba Sc, wamesafiri kwenda nchini Sudan kwaajili ya kushiriki mashindano yaliyoandaliwa na wenyeji wao Al Hilal ya nchini Sudan.

Simba wamealikwa kucheza mechi mbili (2) za kirafiki ambapo mechi ya kwanza watacheza dhidi ya  Asante Kotoko ya Ghana Agosti 28, na Al Hilal ya Sudan Agosti 31, kabla ya kurejea tena Dar Es Salaam kucheza mechi ya tatu ya kirafiki dhidi ya As Arta Solar Septemba 3 ambao itakamilisha ratiba ya mechi za kirafiki.

Je ni nini faida ya mechi hizi za kirafiki.

Mechi za kirafiki zitakuwa na faida kubwa sana kwa upande wa Simba SC kwa maana ya kwamba, mechi hizi zitampa nafasi Kocha Zoran Maki kuona mapungufu yake ni wapi ili aweze kuboresha kabla ya mashindano ya klabu bingwa kuanza.

kwa upande wa wachezaji itawasaidia kupambania namba kwa kumshawishi mwalimu Maki mazoezini, mchezaji kama Victor Akpan ambaye amekuwa bado hajamshawishi mwalimu, huu ndiyo muda wake wa kuonyesha mambo makubwa, ambapo hata kocha Zoran alinukuliwa akisema kuwa “atatumia mechi hizi tatu za kirafiki kumbadilisha Akpan” hii ni kama nafasi ya upendeleo ambayo Akpan amepatiwa ni muda wake wa kuonyesha jambo.

 

Acha ujumbe