Simba VS Vipers Kupigwa Saa 1:00 Usiku Jumanne

Mechi ya Klabu Bingwa ya marudiano kati ya Simba dhidi ya Vipers ya Uganda utapigwa majira ya saa 1:00 usiku katika Dimba la Benjamin Mkapa.

 

Simba VS Vipers Kupigwa Saa 1:00 Usiku Jumanne

Awali mchezo huo ulitarajiwa kupigwa saa 10:00 jioni na sasa CAF imetoa maamuzi kuwa mchezo huo kupigwa majira ya saa moja usiku na ratiba hiyo inatolewa kutoka juu na timu ni kufuata maelekezo tuu.

Na katika hiyo michezo ya makundi, mchezo mmojawapo unapigwa katikati ya wiki na sio Simba tu bali ni timu zote ambazo zinashiriki mashindano haya ya CAF.

Simba VS Vipers Kupigwa Saa 1:00 Usiku Jumanne

Mechi ya kwanza walivyokutana mnyama aliondoka na pointi 3 ugenini baada ya kumtungua Vipers bao 1-0 ambalo lilifungwa na beki wa kati Henock Inonga, hivyo mechi hii vijana wa Roberto wanahitaji ushindi ili wawe kwenye nafasi nzuri.

Acha ujumbe