Simba wageukia kimataifa

Baada ya kukamilisha ratiba ya michuano ya Mapinduzi jana alhamis dhidi ya KVZ, kikosi cha Simba kimerejea Jijini Dar kujiandaa na mashindano ya kimataifa.

Simba wamecheza michezo miwili kwenye kundi C dhidi ya Mlandege ambao walipoteza kwa bao 1-0 na kumaliza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya KVZ.

Simba wageukia kimataifa

Katika kundi C Mlandege amefanikiwa kuvuka hatua ya nusu fainali huku Simba wakishika nafasi ya pili baada ya kuvuna pointi tatu na KVZ wakivuna pointi moja pekee.

Kikosi cha timu hiyo kilianza safari ya kurejea Jijini Dar leo asubuhi kwa kutumia usafiri wa boti ambapo tayari kikosi hicho kimewasili Dar.

Simba wageukia kimataifa

Akizungumza baada ya kutolewa katika mashindano hayo, Kocha Mkuu wa Simba, Juma Mgunda alisema wanarejea Jijini Dar kujiandaa na michuano ya kimataifa.

“Tumeshatolewa kwenye haya mashindano hivyo tutarejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya ligi ya mabingwa Afrika.

“Tulivyokuja kwenye mashindano haya ya Mapinduzi mipango ilikuwa ni kuyatumia kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa lakini tumetolewa hivyo tunaenda kujiandaa Dar.”

Acha ujumbe