SIMBA WAMEWEKA REKODI ITAKAYOISHI MILELE

HATIMAYE yametimia yale ambayo yalikuwa yanazungumzwa kwa muda mrefu. African Football League imezinduliwa kwenye ardhi yenye amani na upendo na klabu ya Simba ndio  wenyeji wa ufunguzi wa michuano hiyo.

Ardhi yenye mvuto kutoka kwa wenyeji na wageni. Ardhi yenye mbegu bora ya ujamaa, hakika Tanzania imetajwa sana kwenye ulimwengu wa soka duniani.simbaHayo, hayajafika bure, bali ni kwa jitihada za za klabu ya Simba ambayo ilianza kuivesha nguo Tanzania miaka minne, mitano iliyopita. Kwa kufanya vema kwenye mashindano ya Afrika.

Hiyo ni hoja hai ambayo watu wanajaribu kuia au kuipoteza bila sababu ya msingi. Kwa pamoja tunapaswa kuwapongeza Simba na kuwatakia kila la heri kwenye mchezo wao.

Watambue tu kuwa siyo rahisi kuwafunga Al Ahly wakiwa wanataka jambo lao, lakini inawezekana kutokana na maandalizi ambayo yatakuwa yamefanywa.simbaWatanzania wote kwa pamoja inapaswa kuungana kwenye hili, kwa kuwa ushindi wa Simba ni ushindi wa taifa na ni ushindi wa kila Mtanzania.

Ushabiki wa klabu zetu ukae pembeni kwa muda, ili kuweza kuunganisha nguvu kwenye jambo hili kubwa na lenye hisia kubwa kwenye mpira wetu

Acha ujumbe