SIMBA WANAZITAKA TATU DHIDI YA GEITA LEO

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unazihitaji pointi tatu za Geita Gold FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa CCM Kirumb, Mwanza

Hiyo ni baada ya wiki iliyopita kushindwa kutamba mbele ya Azam FC na mchezo kutamatika kwa sare ya bao 1-1, Simba wakichomoa kwenye dakika za majeruhi za mchezo.

Ikumbukwe kwamba mchezo uliopita ikiwa nyumbani, ubao wa Uwanja wa CCM Kirumba ulisoma Simba 1-1 Azam FC huku wafungaji wakiwa ni Clatous Chama kwa Simba dakika ya 90 na Prince Dube kwa Azam FC dakika ya 14.

Ikiwa imecheza mechi 13na pointi 30 kibindoni inatarajiwa kumenyana na Geita Gold yenye pointi 16 baada ya kucheza mechi 13.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa mpango mkubwa ni kupata furaha na ushindi jambo ambalo linawezekana.

“Tunahitaji kupata furaha na ushindi kwenye mechi ambazo tunacheza na kuelekea mchezo wetu dhidi ya Geita Gold tunahitaji kupata pointi tatu,”.

Acha ujumbe