Kesho Jumapili Simba watakuwa nyumbabi KMC Complex kuvaana na Simba kwenye mchezo mwingine muhimu kwao msimu huu kwenye harakati zao za kuwania ubingwa na wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na kumbukumbu wawili hao ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza.

Huku viongozi wa Simba wakitoa tahadhari kubwa kwa wapinzani wao hao, wakisema wao wanahitaji ushindi kwenye kila mchezo wanakwenda kwenye mchezo huo wakiwa na sura tofauti kabisa.
Huku wakisema wanaelewa Dodoma Jiji FC imekuwa ikitoa ushindani na matokeo yasiyotabirika inapokutana na timu kubwa. Wamewahi kuwatibua Yanga SC kwa matokeo ya kushangaza na pia kuwapa wakati mgumu Simba SC kwa sare katika michezo ya nyuma. Rekodi hiyo imewajengea sifa ya kuwa “timu hatari kwa vigogo”, jambo linaloongeza tahadhari kwa wapinzani wao.
Wekundu wa Msimbazi wanaingia katika mchezo huo wakiwa na presha ya kuendeleza ushindani mkali katika mbio za ubingwa wa ligi, huku wakijua kuwa makosa madogo yanaweza kuwagharimu pakubwa. Licha ya ubora na kina cha kikosi chao, bado wanatambua kuwa Dodoma Jiji mara nyingi hucheza kwa ujasiri mkubwa wanapokutana na timu kubwa.
Beki wa Mnyama, Nickson Kibabage, amesisitiza kuwa mchezo huo hautakuwa mwepesi kama watu wengi wanavyoweza kufikiria, akibainisha kuwa wapinzani wao wana nidhamu na mpangilio mzuri wa kiuchezaji.



