Simba Yaachana Rasmi na Augustine Okrah

Hatimaye sasa baada ya kudumu kwa mwaka mmoja akiwa Msimbazi, Augustine Okrah na Simba wamemalizana na hivyo hatakuwa tena mchezaji wa klabu hiyo kuanzia sasa.

 

Simba Yaachana Rasmi na Augustine Okrah

Simba walimsajili Okrah kwa matumaini mengi ya kuwa ataenda kutoa kitu ambacho wana msimbazi walikitarajia baada ya kuondokewa na baadhi ya wachezaji wao muhimu akiwemo Luis.

Lakini sasa imekuwa ndivyo sivyo Okrah hakuweza kuthibitisha yale ambayo yalitarajiwa klabuni hapo ukizingatia na kuzongwa na majeraha ya hapa na pale hivyo ikawa ngumu kwa klabu kuendelea nayo.

Timu ya Robertinho sasa ni msimu wa pili mfululizo wanakosa kombe la ligi mbele ya watani wao Yanga, huku wengi wakisema kuwa usajili wanaofanya Msimbazi ndio unawafanya kutofikia malengo yao hata klabu bingwa.

Simba Yaachana Rasmi na Augustine Okrah

Okrah anaondoka klabuni hapo ambapo mnyama anahitajika kufanya usajili mwingine mkubwa eneo la washambuliaji ili aweze kufanikisha kuwania mataji mbalimbali likwemo taji la ligi, FA na klabu bingwa Afrika.

 

 

Acha ujumbe