Klabu ya Simba FC imeanza safari ya kurejea Dar es Salaam kutokea Zanzibar baada ya kutolewa kwenye Kombe la Mapinduzi licha ya kushinda mchezo wao wa jana dhidi ya KVZ kwa bao 1-0.
Simba ambaye alikuwa bingwa mtetezi wa kombe hilo, alishindwa kulitetea baada ya kupoteza mechi yake ya kwanza kwa bao 1-0 dhidi ya Mlandege huku matumaini ya kusalia visiwani kuwa machache.
Baada ya kupoteza mechi ya kwanza mnyama alibakiza mechi moja ya kukamilisha ratiba tuu kwani kwenye kundi hilo tayari Mlandege alikuwa akiongoza kundi hilo kwa alama 4 hivyo hata Mgunda na vijana wake wangeshinda mabao 5 yasingesaidia kitu.
Hivyo Simba wanarejea nyumbani hii leo kuendelea kujiandaa na michuano iliyobaki ikiwemo ya CAF pamoja na Ligi na mchezo wao wa kwanza baada ya kutolewa kwenye Kombe hilo atamenyana na Mbeya City kwa Mkapa.