Klabu ya soka ya Simba imeanza mazoezi yake rasmi leo nchini Dubai ambapo ndipo walipoelekea kwajili ya kuweka kambi ya siku saba.

Klabu ya Simba ambayo ilisafiri jana kuelekea nchini Dubai na timu yenye watu 38 kwajili ya kuweka kambi fupi nchini humo. Klabu hiyo imeangazia kuweka kambi Dubai kwajili yua kujiandaa na michuano ambayo inawakabili katika siku za mbeleni.SimbaTimu hiyo imekwenda Dubai baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la mapinduzi visiwani Zanzibar, Ndipo mwekezaji wa klabu hiyo alipowapa mualiko klabu hiyo kwenda nchini Dubai kwaji ya mapumziko mafupi na kujiandaa kwajili ya michuano mbalimbali.

Baada ya kufika Dubai ni leo rasmi klabu ya Simba imeanza mazoezi yake nchini humo ambapo taarifa ya klabu hiyo ilisema watakaa kwa siku saba. Kocha mpya wa klabu hiyo Roberto Oliviera ameanza programu ya mazoezi kwenye timu hiyo kwa mara ya kwanza.SimbaBaada ya kumalizika kwa kambi hiyo klabu ya Simba itarejea nchini kwajili ya kuendelea na michuano mbalimbali ambayo inawakabili. Kubwa zaidi ni michuano ya ligi ya mabingwa Afrika ambayo klabu hiyo imekua ikiitolea macho zaidi kwa miaka ya hivi karibuni.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa