Simba Yaanza Safari ya Kurejea Jijini Dar es salaam

Baada ya ushindi mkubwa hapo jana wa 3-1 dhidi ya KMC, klabu ya Simba imeanza safari ya kurejea jijini Dar es salaam hii leo kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Tanzania Prisons.

 

Simba Yaanza Safari ya Kurejea Jijini Dar es salaam

Mchezo huo wa Simba dhidi ya Tanzania Prisons utapigwa siku ya Ijumaa katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa 12:15 huku Mnyama akitoka kukusanya pointi saba kanda ya Ziwa.

Baada ya ushindi huo Simba ameendelea kushika nafasi ya pili akiwa na pointi zake 41 akiwa nyuma ya pointi 6 kwa kinara Yanga anayeongoza akiwa na pointi zake 47 kibindoni.

Simba Yaanza Safari ya Kurejea Jijini Dar es salaam

Mgunda na vijana wake watamenyana na Prisons ambao siku zote wakikuatana mechi huwa ngumu na ikiokea mmoja kati yao kashinda huwa ni bao 1 kwa bila ama kwenda sare kabisa.

Katika mechi 5 za mwisho kukutana hakuna ambaye ameshinda zaidi ya goli 1 au hata kwenda sare ya 2-2 hakuna, na hiyo ni kuonyesha kwamba ni kwa jinsi gani hiyo mechi huwa ni ngumu.

Simba Yaanza Safari ya Kurejea Jijini Dar es salaam

Mechi ya mwisho Simba aliondoka na ushindi ambapo bao hilo lilifungwa na Jonas Mkude dakika za jioni za mchezo (86). Je mechi ya marudiano nani kuibuka mbabe kati yao kwa Mkapa?

 

Acha ujumbe