Simba Yabadili Gia Angani

Klabu ya Simba imebadili gia angani na kuacha kutambulisha mchezaji wake saa saba kamili mchana na kutangaza kutangaza mchezaji wake mpya saa kumi na mbili kamili.

Simba inaelezwa ilikua na mpango wa kutambulisha mchezaji mzawa kwa maana wa hapa nchini Tanzania saa saba mchana wa leo, Lakini wamebadilisha baada ya taarifa kuelezwa kuvuja kua watamtambulisha mchezaji gani na kuamua kubadili muda wa kutambulisha mchezaji.

Klabu hiyo imekua ikitambulisha wachezaji wake saa saba mchana ambao ni wapya lakini leo wameamu kubadilisha muda, Huku sababu ikielezwa ni aliyekua kiungo wa klabu hiyo Clatous Chama kutangaza kuachana na timu hiyo na kujiunga na watani zao klabu ya Yanga.

Wekundu wa Msimbazi klabu ya Simba inaelezwa watatambulisha mchezaji mpya wa kigeni ndani ya klabu hiyo saa kumi na mbili kamili jioni ya leo badala ya saa saba mchana, Sababu kubwa ya klabu hiyo kuacha kutambulisha mchezaji mzawa na kutambulisha nyimbo ya kigeni ni kuweka mzani sawa baada ya mchezaji Clatous Chama kutangaza kuondoka klabuni hapo.

Acha ujumbe