Simba Yabeba zote tatu dhidi ya Dodoma

Klabu ya Simba imefanikiwa kutwaa alama zote tatu dhidi ya klabu ya Dodoma Jiji katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa mapema leo katika dimba la Uhuru jijini Dar-es-salaam.

Simba walianza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa mshambuliaji wake Jean Baleke mwishoni mwa kipindi cha kwanza na kuifanya klabu hiyo kwenda mapumziko kwa uongozi wa bao moja kwa bila.simbaKipindi cha pili wekundu wa msimbazi waliendelea walipoishia kwani walionekana kua na njaa ya kupata mabao mengine zaidi kutokana na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye lango la Dodoma Jiji.

Mnyama alipata bao la pili baada ya kuingia kwa mshambuliaji wake Moses Phiri ambaye alianzia nje ambapo mnamo dakika ya 55 akafanikiwa kuongeza bao la pili na wekundu wa msimbazi kuongoza kwa mabao mawili mbele.simbaKlabu ya Simba waliendelea kuliandama lango la Dodoma Jiji baada ya kupata bao la pili na walifanikiwa kutengeneza nafasi nyingi za mabao lakini hawakuweza kuweka mpira wavuni na mchezo huo kumalizika kwa ushindi wa mabao mawili kwa bila.

Acha ujumbe