Klabu ya Simba imefanikiwa kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kuifunga klabu ya Singida Fountain Gate kwa mabao mawili kwa moja katika dimba la Liti mkoani Singida.

Simba wanafanikiwa kushinda mchezo huo ambao ulionekana kua mgumu kuanzia dakika ya kwanza ya mchez mpaka dakika 90 zinamalizika, Mnyama anafanikiwa kuondoka na alama tatu muhimu.simbaWekundu wa Msimbazi walionekana kuanza kwa kasi kuonesha kuhitaji goli la mapema na Singida wakizuia vizuri, Lakini Kibu Denis alifanya kazi nzuri na kumfanya Saidoo Ntibazonkiza kuandika bao la kwanza kwa upande wa Mnyama.

Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa Wekundu wa Msimbazi wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila, Huku kipindi cha pili kikirejea kwa kasi ambapo Singida wakionekana kutafuta zaidi goli la kusawazisha na kufanikiwa ambapo Deus Kaseke akiwapatia bao la kusawazisha.simbaMchezo huo mgumu ulienda hadi dakika za lala salama ubao ukisoma bao moja kwa moja, Ni Moses Phiri ambaye alitokea benchi akiiandikia bao la pili Simba na kuwafanya kuandoka na alama zote tatu na kua na ushindi wa asilimia 100 na kufikisha alama 15 na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa