Simba Yaendelea Kutembeza Panga

Klabu ya Simba inaendelea kutembeza panga katika kikosi chake kwajili ya kusafisha kikosi hicho na kuleta wachezaji wapya ambao watakua bora kuisaidia timu hiyo msimu ujao.

Klabu ya Simba imekua ikipitia kipindi kigumu kwa takribani misimu mitatu sasa hivo lengo kubwa ni kupambana kuhakikisha wanatengeneza timu mpya ambayo itakua na ubora wa kuweza kupambana na kurejesha ubingwa mitaa ya Msimbazi baada ya miaka mitatu.simbaLeo klabu ya Simba imetangaza kuachana na mchezaji mwingine ambaye amedumu ndani ya klabu hiyo kwa takribani kwa misimu mitatu sasa Sadio Kanoute, Lakini anaachwa ndani ya klabu hiyo kutokana na kushindwa kuonesha ubora ambao waliuhitaji ndani ya timu hiyo.

Klabu hiyo kutoka mitaa ya Msimbazi wanaelezwa tayari wameshakamilisha usajili wa wachezaji Wanne wa kigeni na kinachosubiriwa ni kuwatangaza tu, Hii inaonesha namna klabu hiyo imejiandaa kwajili ya kurudisha ubora wao kuelekea msimu ujao.

 

 

Acha ujumbe