Klabu ya Wekundu wa Msimbazi Simba Yazidi kuikandamiza Ihefu katika nafasi ya mwisho baada ya kuifunga kwa bao 1-0 katika mchezo wao wa raundi ya 10 kwenye Ligi kuu ya NBC.

 

Simba Yaididimiza Ihefu Mkiani

Bao hilo lilifungwa na Pape Sakho katika kipindi cha pili dakika ya 62 na kuifanya Simba kujipatia alama 3 ambazo zimemsogeza mpaka nafasi ya pili kwenye ligi huku akiwa na michezo miwili mbele ya Yanga.

Dakika 45 za mwanzo walienda sare ya bila kufungana huku Ihefu wakionekana kutaka kujipatia walau pointi 1 katika uwanja wa Benjamin Mkapa kitu ambacho hakikuwa rahisi kwao kutokana na Msimbazi kuhitaji alama 3 wakiwa nyumbani.

Bado timu ya Juma Mgunda inapata tabu kupata matokeo wanayoyahitaji kutokana na kukosekana mchezaji wao muhimu Cloutus Chama ambaye amefungiwa mechi tatu ikiwemo ya jana, huku akitarajiwa kukosa tena mchezo wa Simba ujao.

Simba Yaididimiza Ihefu Mkiani

Ihefu hali yao imezidi kuwa mbaya wakiwa miani kwenye msimamo huku matumaini yakiwa bado ni kidogo kusalia Ligi kuu endapo wataendelea na mwenendo wa matokeo haya yasiyoridhisha.


aviator

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa