Klabu ya Simba imeifuata Wydad Casablanca kwaajili ya mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Klabu Bingwa Afrika baada ya mnyama kupata ushindi mechi ya kwanza wakiwa kwa Mkapa.
Bao hilo la ushindi lilifungwa na Jean Baleke baada ya kupokea pasi kutoka kwa mshambuliaji Kibu Denis katika dakika ya 31 ya mchezo siku ya Jumapili katika dimba la Benjamni Mkapa.
Licha ya Simba kutengeneza nafasi nyingi za kupata mabao hawakuweza kuzitumia na kusalia na bao hilo hilo moja mpaka kumalizika kwa kipyenga cha mwamuzi dakika 90 za mchezo.
Bado mchezo ni mgumu kwa pande zote mbili na pia kazi bado ni kubwa kwa mnyama akiwa ugenini pale kwa Dimba la Mohamed wa V ambao ndio uwanja wanaoutumia Wydad Casablanca.
Ikumbukwe kuwa vijana wa Robrtinho wakipata sare au ushindi watatinga hatua ya nusu fainali ya klabu bingwa. Je bingwa mtetezi wa kombe hili atakubali kupoteza ubingwa wake hatua ya robo fainali?