Klabu ya Soka ya Simba imekanusha taarifa za aliekua kocha wake wa magolikipa Mohamed Mwarami baada ya kutuhumiwa kwenye usafirishaji wa dawa za kulevya mapema leo.

Golikipa huyo wa zamani wa klabu hiyo ambaye amekutwa na hatia ya kuhusika na usafirishaji wa madawa ya kulevya kupitia mkuu wa udhibiti ya madawa ya kulevya bwana Gerald Kusaya baada ya taarifa ya leo asubuhi.simbaGolikipa huyo ambaye amekua akiifanyia kazi klabu ya Simba kwa vipindi tofauti kama mchezaji na kama kocha wa magolikipa amekubwa na tuhuma hizo akiwa sio mwajiriwa wa klabu ya Simba kitu ambacho klabu hiyo imehitaji kukanusha.

Klabu ya Simba imeeleza wazi kwenye tarifa yake ya Umma kua kocha huyo aliombwa na Uongozi kuitumikia klabu hiyo kwa mwezi mmoja baada ya hapo klabu itatafuta kocha mpya na ndivyo ambavyo klabu imefanya.

Ikumbukwe siku mbili nyuma msemaji wa klabu hiyo amesema watatangaza kocha wa magolikipa na kocha wa viungo siku za hivi karibuni, Jambo ambalo linaonesha wazi Mwarami hakua muajiriwa wa klabu hiyo mpaka anakutwa na tuhuma hizo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa