Simba Yanogesha Tamasha Lao kwa Ushindi

Siku ya jana ya tarehe 03 Agosti Simba SC iliadhimisha tamasha lao la Simba Day ikiwa inatimiza miaka 16 toka kuanzishwa kwake 2009 huku sherehe hizo zikinogeshwa haswa na matukia mbalimbali.

Simba Yanogesha Tamasha Lao kwa Ushindi

Sherehe hizo zilianza mapema kabisa majira ya saa tisa mchana ambapo baadhi ya wasanii waliingia uwanjani kwaaajili ya kutumbuiza na kuwafurahisha mashabiki ambao walijitokeza kwaajili ya kushuhudia timu yao.

Kama ilivyokuwa kawaida ya mashabiki hao wa Lunyasi kujaza uwanja ndiovyo jana ilivyokuwa kwani kufikia majira ya saa kumi jioni uwanja ulikuwa umeshajaa na bado watu wengine walikuwa wamekosa sehemu za kukaa.

Simba Yanogesha Tamasha Lao kwa Ushindi

Simba ilitambulisha wachezaji wao ambao wamewasajili msimu huu kama vile, Awesu Awesu, Debora, Joshua Mutale, Kijiri na wengine kibao ambao wamejiunga na klabu, lakini pia benchi zima la ufundi lilitambulishwa hapo jana pamoja na kocha mpya Davids Fadlu ambaye atakinoa kikosi hicho msimu huu.

Baada ya hapo Mnyama alikipiga mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda ambao ndio walikuwa wamealikwa na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye kipindi cha pili cha mchezo baada ya kwenda dakika 45 bili kufungana.

Simba baada ya kucheza jana anajiandaa na mchezo wa ngao ya jamii ambao utapigwa tarehe 8 mwezi huu yaani siku ya Nane Nane kutakuwa na Kariakoo derby mchezo ambao utapigwa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku.

Simba Yanogesha Tamasha Lao kwa Ushindi

Je kwa kikosi cha jana na jinsi ambavyo wamecheza wataweza kumfunga Yanga ambaye amekuwa na msimu bora na kikosi bora? Beti na meridianbet mechi zinazoendelea sasa.

Acha ujumbe