Simba Yapasuka 5-1 Kwa Mkapa Jana

Mechi ya Derby kati ya Simba dhidi ya Yanga ilimalizika kwa vijana wa Gamondi kupata ushindi mkubwa kabisa wa mabao 5-1 baada ya dakika 90 za mpira kumalizika.

 

Simba Yapasuka 5-1 Kwa Mkapa Jana

Mechi hiyo ilipigwa majira ya saa 11:00 jioni ambapo mwenyeji wa mchezo alikuwa Simba huku akifanya mabadiliko langoni kwa kumuingiza Aishi Manula mbaye hakuwa uwanjani kw amuda mrefu.

Yanga walitamngulia kupata bao katika dakika ya 03 kupitia kwa Kennedy Musonda akifunga kwa kichwa huku Kibu Dennis akiisawazishia Msimbazi dakika ya 09 ya mchezo kabla ya mapumziko.

Waliporejea kipindi cha pili ndipo mambo yalipobadilika na hatimaye kuruhusu mabao mengine manne kupitia kwa Aziz Ki, Max Mpia mawali na Pacome kwa bao la penati na kukamilisha mabao matano.

Simba Yapasuka 5-1 Kwa Mkapa Jana

Mara ya mwisho Yanga kumfunga Simba mabao matano ilikuwa mwaka 1968 hivyo historia imejirudia mnyama kufa kwa mabao mengi miaka ya hivi karibuni kwenye derby.

Kwa ushindi huo hapo wa jana Yanga anasalia kileleni kwenye msimamo wa ligi akiwa na pointi zake 21 huku vijana wa Robertinho wakiwa nafasi ya tatu na pointi zao 18 na mchezo mmoja mkononi.

 

Acha ujumbe