Simba yarejea Dar kibabe

Baada ya kucheza mechi tatu Kanda ya Ziwa, kikosi cha Simba kimerejea Dar leo jumanne kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda imefanikiwa kuvuna pointi saba katika michezo mitatu dhidi ya Kagera Sugar (1-1), Geita Gold (0-5) na KMC (1-3).

Simba yarejea Dar kibabe

Kikosi hicho kimerejea Jijini Dar leo jumanne kikitokea Jijini Mwanza ambapo kilianza safari leo asubuhi baada ya mchezo wao wa mwisho wa jana jumatatu dhidi ya KMC.

Simba yarejea Dar kibabe

Timu hiyo mpaka sasa imefanikiwa kukusanya pointi 37 baada ya kucheza mechi 18 za ligi na kufanikiwa kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Acha ujumbe