Simba Yaruhusiwa Kutumia Uwanja wa New Amaan Zanzibar

BODI ya Ligi imeweka wazi kwamba kuna maboresho kwenye Kanuni za ligi msimu wa 2024-25 ambapo zinaruhusu timu za Ligi kuu ikiwemo Simba na Yanga kutumia viwanja vya Unguja na Pemba visiwani Zanzibar ikiwa vitakidhi vigezo. Jisajili hapa kuwa wa kwanza kushinda Mamilioni ya Meridianbet kila siku.

Almas Kasongo alisema kuwa baadhi ya kanuni za ligi msimu ujao wa 2024/25 ni kuwa uwanja ambao hautakuwa na viti elfu tatu (3,000) kwa ajili ya mashabiki havitatumika kwenye michezo ya Ligi Kuu.

“Jana nimepokea barua ya timu ya Ligi Kuu kutumia uwanja wa Zanzibar kama uwanja wao wa nyumbani. Timu yeyote ya Tanzania Bara, ikiamua kutumia uwanja wowote visiwani (Unguja/Pemba) ruksa,” alisema Kasongo.

Beti na Meridianbet kwa ushindi mkubwa na odds kubwa, Ligi  zinakaribia kuanza,  usije kupishana na gari la Mshahara.

Itakumbukwa kuwa, msimu uliopita Simba iliandika barua kwa Bodi ya Ligi kuomba uwanja wa Amaan kuwa uwanja wao wa nyumbani, lakini kulingana na kanuni za ligi zilizokuwepo, Simba haikuruhusiwa kutumia uwanja huo.

Lakini kukamilika kwa uwanja wa KMC FC Mwenge unaipa nafasi Simba kuchagua watumie uwanja huo, au wapeleke mechi zao Unguja.

Hiyo itakuwa faidi kwa mashabiki wa Zanzibar kuona timu yao, na Simba itapata mapato, lakini suala ni moja tu endapo muitiko utakuwa mdogo wa mashabiki.

Kasino ya Mtandaoni usipange kuacha kucheza, Meridianbet wameakuandalia Maokoto na bonasi za kasino kibao.

Acha ujumbe