WAKITARAJIA kuingia kambini, Simba wameendelea kushusha vifaa ambapo wamemtambulisha rasmi, Augustine Okrah raia wa Ghana.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Simba imeeleza kuwa “Mchezaji mkubwa mwenye hadhi ya kucheza timu kubwa kama Simba, Augustine Okrah ni Mnyama.”

Kikosi cha Simba kinatarajia kuingia kambini leo Jumatano tayari kwa ajili ya maandalizi ya safari ya kesho alhamis kuelekea nchini Misri kwa ajili ya kambi yao.

Okrah atajiunga na kikosi hicho ambacho kinatarajia kuweka kambi kwenye mji wa Ismailia, nchini Misri kwa ajili ya kujiandaa na msimu ujao wa 2022/23.

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa