Simba Yashusha Mashine Nyingine

Klabu ya Simba imefanikiwa kusaini mashine nyingine kuelekea msimu ujao ambapo wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa klabu ya St. Lupopo kutoka nchini DRC Congo Valentino Nouma.

Simba wamemsajili beki huyo mwenye umri wa miaka (24) ambaye amefanikiwa kucheza kwa kiwango bora sana kunako ligi kuu ya DRC Congo, Jambo ambalo liliwavutia viongozi wa Mnyama na kuamua kumsajili beki huyo ambaye atakuja kuleta ushindani kwa beki Mohamed Hussein Zimbwe Jr.SimbaWekundu wa Msimbazi wamedhamiria kwa kiwango kikubwa kuhakikisha wanairejesha timu hiyo kwenye kilele cha ubora ambacho klabu hiyo imekua nayo miaka minne hapo nyuma, Ambapo ndio imekua sababu kubwa ya kuhakikisha wanaingia sokoni na kusajili wachezaji wenye ubora mkubwa.

Mpaka wakati huu klabu ya Simba imeshafanikiwa kukamilisha sajili za wachezaji saba wa kigeni, Huku utambulisho wa Valentino Nouma ambaye ametambulishwa leo raia wa Burkina Faso ndio amekamilisha orodha ya wachezaji saba wakigeni katika orodha hiyo.

SimbaBeki Mohamed Hussein Zimbwe Jr amekua na ubora mkubwa sana kwa zaidi ya miaka nane sasa ndani ya klabu ya Simba, Kusajiliwa kwa Nouma katika nafasi hiyo ni wazi klabu hiyo imepanga kuleta ushindani mkubwa katika nafasi hiyo lakini pia itaongeza machaguo kwa mwalimu Fadlu Davids.

Acha ujumbe