Simba Yashusha MVP wa Ivory Coast

Klabu ya Simba imefanikiwa kunasa saini ya kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast kutoka klabu ya Stella Abidjan anayefahamika kwa jina la Jean Charles Ahoua mwenye umri wa miaka 22.

Jean Charles Ahoua ambaye amekua mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliomalizika ametambulishwa leo saa 12 jioni na klabu ya Simba, Huku ikielezwa ndio mchezaji ambaye anakuja kurithi mikoba ya kiungo Clatous Chama ambaye ametimkia klabu ya Yanga.

Simba wameingia sokoni msimu huu kuhakikisha wanarejesha heshima ya klabu hiyo kutokana na kutokufanya vizuri kwa klabu hiyo misimu mitatu iliyomalizika, Huku kiungo Ahoua akionekana ni moja ya wachezaji ambao wataweza kurejesha makali ya mnyama kuelekea msimu ujao.

Mchezaji Jean Charles Ahoua ambaye anafahamika kama kiungo wa ushambuliaji mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza mashambulizi, kuzuia  pale ambapo timu yake inaposhambuliwa, Lakini bila kusahau uwezo wake mkubwa wa kufunga ambapo msimu uliomalizika amefunga mabao 12 akifanikiwa kutoa pasi 9 za mabao.

Klabu ya Simba mpaka sasa imeshafanikiwa kusajili wachezaji watatu wa kigeni ambao ni Joshua Mutale, Steven Mukwala, pamoja na kiungo Jean Charles Ahoua ambaye ndio ametambulishwa leo na wekundu hao wa msimbazi wameonekana kupania kwelikweli kwenye usajili na sio usajili tu usajili makini.

Acha ujumbe