Klabu ya soka ya Simba imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya CSKA Moscow uliopigwa katika mchezo uliopigwa nchini Dubai mapema leo hii.
Klabu ya Simba ambayo imeweka kambi nchini Dubai kwajili ya kujiandaa na michuano mbalimbali ambayo inafuata siku za mbeleni wamefanikiwa kucheza mchezo wao wa pili wa kirafiki leo tangu waende nchini Dubai tarehe saba nwezi huu.
Klabu ya Simba imefanikiwa kutoka nyuma katika mchezo huo wa kirafiki na kusawazisha mabao mawili waliyotanguliwa na CSKA Moscow. Wekundu wa msimbazi walitanguliwa mabao mawili kwa bila na kufanikiwa kusawazisha mabao hayo kupitia kwa mchezaji Habib Kyombo.
Wekundu wa Msimbazi wamefanikiwa kumaliza mchezo wao wa pili wa kirafiki kwa kupata matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili baada ya kukubali kichapo katika mchezo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya klabu ya Al Dhahra ya nchini Dubai.
Baada ya mchezo wa leo klabu ya soka ya Simba sasa itarejea nchini Tanzania baada ya kambi yake ya siku saba kumalizika nchini Dubai, Huku wakifanikiwa kupata michezo miwili ya kujipima uwezo dhidi ya Al Dhahra pamoja na CSKA Moscow.


