Simba Yatoa Suluhu Dhidi ya Jamus Kombe la Kagame

Bingwa wa kihistoria wa Kombe la CECAFA Kagame, Simba imejikuta ikianza kupiga hesabu za vidole kufuzu hatua ya nusu fainali baada ya kutoka suluhu ya pili mfululizo, safari hii ikiwa dhidi ya Jamus SC ya Sudan Kusini kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Kigali.

Simba Yatoa Suluhu Dhidi ya Jamus Kombe la Kagame

Kufuatia matokeo hayo, Wekundu wa Msimbazi wamefikisha pointi mbili pekee na kuacha hatma yao mikononi mwa mechi ya mwisho ya hatua ya makundi.

Kocha Steve Barker alianza mchezo huo akiwa amefanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi chake huku Mothusi Cooper, ambaye yupo kwenye majaribio, akiwa miongoni mwa walioanza.

Wachezaji wengi waliokuwa tegemeo la kikosi cha kwanza walianzia benchi. Kipindi cha pili Barker aliongeza nguvu kwa kufanya mabadiliko manne kwa wakati mmoja, akiwaingiza Keletso Makgalwa, Ibrahim Doumbia, Yusuph Kagoma na Rushine De Reuck, kabla ya baadaye kuwaingiza Nickson Kibabage na Libasse Guaye.

Mabadiliko hayo yaliifanya Simba kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha pili, lakini ilishindwa kutumia nafasi ilizozitengeneza na kupata bao la ushindi.

Je Wekundu hao wa Msimbazi wataishia nafasi ya ngapi kwenye michuano hii inayoendelea kule Rwanda?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.