Simba Yatua Zambia, Mrithi wa Onana Anatafutwa

SIMBA SC wana jambo lao msimu huu, maafisa wa timu hiyo inaelezwa wametia timu Zambia kufuatilia saini ya winga wa Power Dynamos ambaye amekuwa na msimu mzuri katika ligi hiyo. Meridianbet wanakupa nafasi  ya kuwa tajiri kwa kubashiri mechi  nyingi.

Simba ikumbukwe kuwa msimu ulioisha imewahi kukutana na timu hiyo, katika mchezo wa hatua ya pili wa kufuzu makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kinda huyo aliwappa wakati mgumu sana Mohammed Hussein na Shomary Kapombe.

Inaelezwa kwamba muda wowote kuanzia sasa klabu ya Simba itakamilisha usajili wa winga wa Power Dynamos,raia wa Zambia Joshua Mutale (22), Utajiri rahisi unaupata Meridianbet pekee, jisajili uwe moja ya mabilionea wakubwa.

Viongozi wa Simba wako Zambia kukamilisha dili hili, na hii ni kamati mpya ya usajili ya timu hiyo ikiwa tayari ipo kazini.

Msimu uliopita Joshua Mutale alifunga goli 8 kwenye ligi ya Zambia, anapenda kuvaa jezi namba 7 ambayo jezi hiyo huvaliwa na Willy Essomba Onana ambaye, msimu uliopita hakuwa na makali sana.

Wakati huo huo mshambuliaji wa Singida Black Stars, Ismail Mgunda yupo katika mazungumzo na Simba ili kujiunga na kikosi hicho msimu ujao. Mgunda aliyemaliza na mabao sita ya Ligi Kuu, amefuatwa na viongozi wa Simba ili akaichezee, ikielezwa mazungumzo yanaendelea Singida ikiwa tayari kumuachia.

Acha ujumbe