SINGIDA Big Stars ambao wamepanda daraja msimu uliomalizika hivi karibuni wameendelea kujiimarisha na sasa wamemtangaza Benedict Haule kuwa kipa wa timu hiyo akiungana na Metacha Mnata.

Haule alikuwa ni mali ya Azam FC ambaye alikuwa anacheza Tanzania Prisons kwa mkopo amekula kandarasi ya mwaka mmoja ya kushirikiana na Metacha ambaye alikuwa kipa wa kwanza kutambulishwa.

Singida Big Bullets Yamnasa Kipa wa Azam

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Singida Hussein Masaza alisema isajili wa Haule ni kama kuongeza nguvu kwenye kikosi hicho ambacho kina malengo ya kufanya makubwa zaidi msimu ujao.

“Tumempa mkataba wa mwaka mmoja ambao utakuwa na kipengele cha kumuongezea zaidi kutokana na mchango wake kwenye timu yetu”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa