Klabu ya Singida Big Stars imefanikiwa kupata ushindi dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya NBC  mzunguko wa pili katika dimba la Sokoine mkoani Mbeya.

Klabu ya Tanzania Prisons wakiwa nyumbani wamekubali kupokea kichapo cha mabao mawili kwa moja dhidi ya walima alizeti kutoka mkoani Singida klabu ya Singida Big Stars, Hivo kuwafanya wajelajela kuanza vibaya mzungo wa pili wa ligi ya NBC.singida big starsKlabu ya Singida Big stars ilijpatia ushindi huo baada ya kucheza vizuri kuanzia dakika ya kwanza na kuwafanya kupata bao la mapema katika mchezo huo, Dakika ya tano tu ya mchezo kiungo mwenye asili ya Brazil Bruno Gomes anaipatia timu hiyo bao la kuongoza.

Klabu hizo zilifanikiwa kwenda mapumziko Singida wakiwa mbele kwa bao moja kwa bila dhidi ya Prisons, Kipindi cha pili kilirejea kwa Singida kuendelea kua na kasi na kutafuta bao la pili mpaka pale dakika ya 57 Meddie Kagere kufunga bao la pili huku bao la kufutia machozi la wajelajela likifungwa na Jumanne Elifadhili dakika ya 79 kwa mkwaju wa penati.singida big starsKlabu ya Singida Big Stars imefanikiwa kufikisha alama 30 baada ya kucheza michezo 16 na kuendelea kusalia nafasi ya 4 kwenye msimamo huku Tanzania Prisons wakibaki na alama zao 15 kwenye nafasi ya 11.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa