UONGOZI wa kikosi cha Singida Big Stars umefunguka kuwa hawataki masihala kwa msimu ujao kwani wanahitaji kumaliza katika nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi. 

Mtendaji Mkuu wa timu ya Singida Big Stars, Muhibu Kanu amefunguka kuwa mipango yao ni kumaliza kwenye nafasi tatu za juu kwenye msimamo wa ligi kwa msimu ujao.

“Hakuna kingine zaidi ya kumaliza katika nafasi tatu za juu ikiwezekana kubeba kabisa ubingwa, kwani sisi tunakuja katika ligi kushindana sio kushiriki.

“Na hilo limethibitika kutokana na usajili bora tuliofanya wa wachezaji wenye uzoefu na kiwango kikubwa cha kucheza soka.

“Wapinzani wajiandae vema, hatutaki kufanya masihara kabisa kwa msimu ujao ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ushindani uliokuwepo wa timu.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa