Uongozi wa klabu ya Singida Big Stars umetamba kuwa kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga watakuwa na sapraiz ya mchezaji mpya kwenye kikosi.
Ikumbukwe dirisha dogo la usajili lilifunguliwa Desemba 15, 2022 na linatarajiwa kufungwa Januari 16 mwaka huu.
Tayari Singida wamefanya usajili wa wachezaji wawili ambao ni Ibrahim Ajibu kutoka Azam FC na Nickson Kibabage akitokea Mtibwa Sugar.
Muhibu Kanu ambaye ni Mratibu wa Singida Big Stars, amesema kuwa “Tunawaheshimu Yanga ni timu kubwa pia ina historia kubwa kwenye soka la Tanzania.
“Haya ni mashindano ya Mapinduzi na sisi mipango yetu ni kuhakikisha kwa mara ya kwanza tunafanya vizuri zaidi uwanjani na kusonga mbele.
“Ajibu ni mchezaji ambaye tulimwamini na tumemsajili, tuna imani atafanya vizuri na leo hii huenda akawa kwenye kikosi lakini kuna sapraiz ya sura mpya kwenye kikosi chetu, watu watarajie kuiona leo uwanjani na kwenye TV.”