Klabu ya soka ya Singida Big Stars kutoka mkoani Singida inayoshiriki ligi kuu ya NBC imeachana na mshambuliaji wake raia wa Burundi Amis Tambwe na kumuwinda mshambuliaji wa Azam Shaban Iddi Chilunda.

Klabu ya Singida Big Stars ineonekana kua makini kwenye dirisha dogo la mwezi Januari baada ya kusajili wachezaji kadhaa ikiwemo beki kutoka Mtibwa Sugar Nickson Kibabage na taarifa zinaeleza kua wameshamalizana na Ibrahimu Ajibu kutoka Azam.singida big starsKlabu hiyo inayoshika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC imeachana na mshambuliaji wake Amis Tambwe ambaye alikua miongoni mwa wachezaji walioipandisha timu hiyo daraja, Na hiyo ni kwasababu wapo mbioni kumalizana na mshambuliaji asiekua na nafasi ya kudumu ndani ya Azam Shabani Iddi Chilunda.

Singida Big Stars wana mipango mikubwa kuelekea ugwe ya pili ya ligi kuu ya NBC na zaidi ni kuhakikisha wanamaliza katika nafasi nne za juu ili kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa katika msimu unaofata.singida big starsKlabu hiyo ambayo imekua na kiwango kizuri msimu huu baada ya kupanda kwenye ligi kuu ya NBC mpaka sasa wanaonekana wana wakati mzuri, Ikumbukwe baadhi ya viongozi wa klabu hiyo walieleza mipango yao ni michuano ya Afrika mwakani na ndio sababu kubwa klabu hiyo kufanya sajili za kutosha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa