Singida Big Stars Yaibamiza Kagera Sugar.

Klabu ya Singida Big Stars imefanikiwa kuifunga klabu ya Kagera Sugar wakiwa katika dimba lao la nyumbani Kaitaba mkoani Kagera kwa jumla ya mabao mawili kwa moja.singida big starsWenyeji wa mchezo huo klabu ya Kagera Sugar walianza kupata kupata goli kupitia kwa mshambuliaji wao mahiri Hamis Kiiza alieifungia klabu hiyo bao la kuongoza ambapo bao hilo lilidumu mpaka timu hizo zinaenda mapumziko.

Kipindi cha pili Singida Big Stars wao walikuja kivingine wakiwa wanashambulia kwa kasi ili kusawazisha bao hilo mpaka pale dakika ya 51 Mbrazil Bruno Gomes alipoisawazishia klabu hiyo na mchezo kua bao moja kwa moja.singida big starsKlabu hizo ziliendelea kutafutana kwa kushambuliana kwa zamu ili kupata alama tatu mpaka dakika ya tisini Bruno Gomes aliporudi kambani kwa mara ya pili na kuiandikia Singida big stars bao la pili na la ushindi kwenye mchezo huo.

Walima alizeti walifanikiwa kumaliza kupata ushindi katika mechi hiyo na kusogea kwa nafasi tatu juu katika nsimamo wa ligi kuu kutoka nafasi ya 10 mpaka nafasi ya saba na alama zao 11.

Acha ujumbe