Klabu ya Singida Big Stars imeendeleza wimbi la Ushindi baada ya leo kuifunga klabu ya Polisi Tanzania katika mchezo uliopigwa katika dimba la Black Rhino wilayani Karatu mkoani Manyara.

Singida Big Stars wanapata ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuifunga Polisi leo kwa bao moja kwa bila, Goli lililowekwa kimiani na mshambualiaji wa zamani wa klabu ya Simba Meddie Kagere katika dakika ya 22 ya mchezo.singida big starsWalima alizeti hao wakiwa ugenini wamefanikiwa kupata alama tatu muhimu na kusogea hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC baada ya kufikisha alama 17 kwenye michezo tisa waliyocheza.singida big starsKlabu ya Singida Big Stars ni miongoni mwa timu ambazo zilitarajiwa kuleta ushindani mkubwa kunako ligi ya NBC na ndicho wanachokifanya hivi sasa, Hiyo imekuja baada ya kulingana alama na Simba na Azam huku wakishika nafasi ya nne kwenye msimamo.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa