Singida Big Stars wapewa mwaliko Mapinduzi Cup

Singida Big Stars ni moja ya timu iliyowekwa katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi January 1 hadi 13, 2023 visiwani Zanzibar.

Msimu uliopita Simba walifanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo baada ya kuifunga Azam FC kwenye fainali kwa bao 1-0.

Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF) imeeleza kuwa timu zilizoteuliwa visiwani Zanzibar ni Sita.

Singida Big Stars wapewa mwaliko Mapinduzi Cup

 

Timu hizo ni KVZ, Mlandege, Malindi, KMKM, Chipukizi na Jamhuri huku timu tano zikitoka Bara na moja kutoka Burundi.

Timu za Bara ni Yanga, Simba, Azam, Namungo, Singida Big Stars na timu ya Eagle Noir kutoka Burundi.

Acha ujumbe