Ligi kuu ya NBC itaendelea hii leo kwa michezo miwili ambapo mchezo wa kwanza ni kati ya Singida FG dhidi ya Mashujaa ambao ndio wenyeji wa mchezo huo.
Mehi hiyo inatarajiwa kupigwa majira ya saa 10:00 jioni katika dimba la Lake Tanganyika huu ukiwa ni mchezo wa 8 kwa mwenyeji na mchezo wa 9 kwa mgeni wake mpaka sasa.
Mechi iliyopita Mashujaa wamepoteza mchezo wao wakiwa nyumbani wakati kwa upande wa Walima Alizeti wao walipata sare mchezo wao uliopita.
Mwenyeji kwenye mechi hizo alizocheza ameshinda mechi mbili, sare mbili na kupoteza mechi tatu, wakati kwa upande wa Singida wao wameshinda mechi zao mbili, sare tatu na vipigo vitatu.
Tofauti ya pointi kati yao ni pointi moja pekee huku leo hii kila timu ikihitaji ushindi kupanda nafasi inayofuata kwenye msimamo wa ligi. ODDS KUBWA zipo mechi hii pale Meridianbet, inia na ucheze.