Agosti 4, mwaka huu Singida inatarajia kufanya tamasha lao kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha ambapo licha ya kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Zanaco pia watawatambulisha nyota wao.

Singida, Singida Kutambulisha Mastaa Singida Day, Meridianbet

Akizungumzia maandalizi yao, Mtendaji Mkuu wa Singida Big Stars, Muhibu Kanu amesema kuwa “Kwa sasa kikosi kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu wetu mpya ujao.

“Kikubwa zaidi kwa sasa ni kwamba tunajiandaa na siku ya Singida Big Stars ambapo tutakuwa na utambulisho wa wachezaji wetu ambao hatujawatambulisha.

“Unajua watu hawajui kama kuna wachezaji bado hatujawatambulisha ila yale wanayouliza kuhusu usajili wa kina Kagere (Meddie) na wengine basi waje kwa wingi ili wajue wachezaji wetu wa msimu ujao.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa