Kikosi cha Singida Big Stars kipo tayari kwa ajili ya kuhakikisha kwenye mzunguko wa pili kinapambania malengo ya timu.

Singida ambao ni wageni kwenye ligi kuu kwa msimu huu katika michezo 15 tayari wamekusanya pointi 27 huku wakishika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi.

Singida wapo tayari kupambania malengo yao

Kikosi hicho kinanolewa na Kocha Mkuu, Hans Van De Pluijim kimeonyesha kiwango kizuri katika michezo 15 ya mzunguko wa kwanza.

Kupitia ukurasa wao, timu hiyo imeeleza “Tumemaliza salama mzunguko wa kwanza kwa mafanikio makubwa.

“Tupo tayari kwa mzunguko wa pili na kuongeza kasi zaidi ya kupambania malengo yetu ya msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa